Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya mapumziko ya siku nne kumalizika, kikosi cha Simba kimerejea mazoezini ili kujiandaa na mechi mbili zilizobakia za Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal, lakini pia maandalizi ya msimu mpya.
Mazoezi hayo yamefanyika kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu, Robert Oliveira 'Robertinho’ ambaye alisema wachezaji wote wameshiriki programu hiyo.
Robertinho alisema anaimani mchezo ujao watavuna pointi tatu ili kumaliza ligi kwa heshima.
"Tunajiandaa vizuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwa kuvuna pointi sita ili kumaliza ligi kwa heshima na kuanza kujiandaa kwa msimu mpya," alisema kocha huyo.
Aliongeza anaimani na wachezaji wake watapambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo hiyo kwa lengo la kuwapa furaha wanachama na mashabiki wa klabu hiyo ambao waliwasapoti wakati wote.
Alisema pia mipango kuelekea msimu mpya imeshaanza na wanawaahidi mashabiki watawafuta machozi kutokana na kushindwa kufikia malengo msimu huu.
Post a Comment