Simba yamzuia Tshabalala kwa Sh300 Milioni

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kikosi cha Simba kinaendelea kujifua kwa ajili ya mechi mbili za mwisho za Ligi Kuu Bara msimu huu dhidi ya Polisi Tanzania Coastal Union, lakini huku mabosi wa kikosi hicho wakiendelea na utekelezaji wa mapendekezo ya kocha wa timu hiyo ili kuunda skwadi la nguvu kwa msimu ujao.


Katika kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, mabosi hao wameamua kumzuia beki wa kushoto na nahodha msaidizi wa kikosi hicho, Mohamed Hussein 'Tshabalala' kwa kumwekewa Sh 300 Milioni mezani ili asiende klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini iliyokuwa inammnyemelea ili imsajili.


Ipo hivi. Tshabalala amebakiza mechi mbili tu kuuaga msimu huu na kumalisha mkataba wa alionao kwa sasa, lakini ni mmoja wa mabeki ambao Kocha Roberto Oliveira 'Robertinho' anayetaka kuona anasalia kikosini na fasta mabosi wa klabu hio wameamua kumpa mkataba mpya wenye dau nono.


Nahodha huyo msaidizi aliwapa kazi ngumu mabosi wa timu hiyo kumbakiza Msimbazi kutokana na ofa kubwa aliyokuwa amepewa na Kaizer Chiefs iliyowekwa dau la Sh 400 Milioni na mshahara wa Sh 30 Milioni kwa mwezi, lakini walipambana na kumalizana naye na beki huyo kusaini dili jipya.


Inaelezwa Simba ilishtuka mapema baada ya taarifa za kutakiwa kwa Tshabalala na kuamua kukaa naye mezani na kupata muafaka katika majadiliano ya muda mrefu chini ya menejimenti yake na hatimaye akakubali kusaini dili hilo la miaka mitatu kwa kupewa Sh 300 Milioni na mshahara wa Sh 10 Milioni. Chanzo cha kuaminika kutoka klabu ya Simba kililiambia Mwanaspoti kuwa, staa huyo ataendelea kubaki Simba baada ya makubaliano hayo kukamilika na kusaini mkataba mpya.


"Haikuwa rahisi kwani, tayari Tshabalala alikuwa na ofa kubwa lakini viongozi wamekaa naye na kufanikiwa kumshawishi ili aweze kuendelea kuitumikia Simba kwa mafanikio kama alivyofanya tangu amejiunga na timu hii akitokea Kagera Sugar," kilisema chanzo hicho.


Kwa dili hilo jipya, Tshabalala aliyejiunga na Simba msimu wa 2014/15 akitokea Kagera Sugar, atakuwa klabuni hapo hadi mwishoni mwa msimu wa 2025-2026 na kwa maana hiyo ndoto ya timu zilizokuwa zikimtaka kufa rasmi.


Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alipotafutwa ili kuthibitisha juu ya taarifa hiyo ya Tshabalala kupewa mkataba mpya na kuitosa Kaiozer Chiefs, alisema uongozi unapambana kuhakikisha wachezaji wote ambao mikataba yao inaisha wabaki kama mapendekezo ya kocha.


"Mazungumzo baina yetu beki kisiki wa Taifa Stars na Simba, Tshabalala yanaendelea vizuri na hakuna chochote kitakachoharibika. Wote tunafahamu ubora wa nahodha msaidizi, hivyo sio rahisi kuruhusu aondoke.” alisema Ahmed Ally.


Katika miaka tisa ambayo Tshabalala ameitumikia Simba tangu alipojiunga nayo ametoa mchango wake kuiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara nne, mataji mawili ya ASFC, kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili tofauti na robo nyingine ya Kombe la Shirikisho.


Chanzo: Mwanaspoti

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post