Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Tangu mwanzoni mwa juma hili Uongozi wa SImba SC umeonesha dhamira ya kuanza kufanya kazi ya usajili, huku baadhi ya mabosi wa klabu hiyo wakikiri kuwa bize na vikao vya kwa nyakati tofauti kupanga bajeti ya msimu ujao, sambamba na kutathimini ripoti ya kocha na usajili mpya.
Taarifa za za ndaani kabisa kutoka katika klabu hiyo ya Mismbazi ni kwamba tayari Viongozi wa Simba SC wameingia sokoni wakijiandaa kumng’oa kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Rwanda.
Kiungo huyo ambaye anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na Simba ni Leandre Willy Onana (23) anayekipiga Rayon Sports na kwa sasa ndiye kinara wa mabao wa katika Ligi Kuu ya Rwanda akifunga 15 na kuasisti 10.
Simba imepania kurejesha ufalme baada ya kukosa mataji katika misimu miwili mfululizo mbele ya watani wao, Yanga na katika kufanikisha hilo imeamua kuingia sokoni kusajili mastaa wapya ambapo kocha mkuu wa kikosi hicho, Roberto Oliveira anataka mchezaji mpya kwenye kila eneo.
Uongozi wa Simba upo tayari kumtimizia kocha huyo kutoka nchini Brazili mahitaji yake na sasa umeanza mazungumzo na wachezaji wanne ambao Robertinho amewapendekeza.
Mbali na Kiungo huyo Mshambuliaji, kuna beki na nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ beki wa kati Thierry Manzi (26), ambaye kwa sasa yuko Ubelgiji kwenye mazungumzo na moja ya timu ya huko, huku Robertinho amewaambia mabosi wa Simba kuhakikisha wanamleta bongo kwani anaamnini ataongeza kitu kwenye ukuta wake na anamfahamu Vyema wakiwahi kufanya kazi pamoja Rayon.
Manzi ana uzoefu wa kutosha na amewahi kuwa nahodha wa APR na Rayon na kutwaa nao mataji pia amewahi kucheza Gerogia katika timu ya FC Dila pia mwaka jana alikuwa FAR Rabat ya Morocco lakini baadae akaomba kuondoka kutokana na mambo ya kimkataba na kurejea Rwanda alipojiunga na AS Kigali.
Kwa kiungo Mshambuliaji Onana anasifika kwa kasi, chenga na stamina akiwa na mpira lakini pia ni mtaalamu wa kufunga akitumia zaidi mguu wa kulia.
Simba ina nafasi kubwa ya kumpata Onana kutokana na kuwa mtu wa karibu zaidi na Robertinho na taarifa za kuaminika ilizonazo zinaeleza, wawili hao meneja wao ni mmoja.
Ukiachana na hao, kuna wachezaji wengine wawili ambao Simba tayari imewavuta Dar es Salaam kwa mazungumzo na wapo hotelini hadi sasa na viongozi wamefanya siri kubwa.
Mapema kocha Robertinho alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema anataka kuitengeneza Simba ambayo itakuwa tishio zaidi ya ilivyokuwa msimu huu ambapo iliishia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kutolewa kwa penalti na Mabingwa watetezi Wydad Casablanca iliyotinga fainali dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Katika Ligi Kuu licha ya kumaliza nafasi ya pili, lakini ndio timu yenye mabao mengi ikifunga 66 na kuruhusu 15 tu, huku nyota wake watatu wakiongoza orodha ya waliopiga hat trick hadi sasa akiwamo nahodha John Bocco, Saido Ntibazonkiza na Jean Baleke.
Taarifa zinaeleza kuwa kuna wachezaji wawili kutoka Ligi ya DR Congo ambao Simba tayari imewashusha Dar es Salaam na kuwafungia hotelini wakiendelea na mazungumzo ya kuwapa mikataba na baada ya hapo watawatambulisha.
Lakini timu hiyo kwa kuanzia imepanga kuachana na mastaa wake, Mohamed Ouattara, Agustine Okrah, Gadiel Michael, Beno Kakolanya, Peter Banda, Ismail Sawadogo na Habibu Kyombo muda wowote kuanzia sasa kutokana na sababu mbalimbali.
Post a Comment