Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Benchi la ufundi la Simba limeweka wazi kuwa hesabu ambazo zipo kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye mechi zote zilizobaki kwa kuwa bado wapo kwenye vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara uliopo mikononi mwa Yanga.
Ni pointi 63 wanazo kibindoni huku watani zao wa jadi Yanga wakiwa na pointi 68, nafasi ya kwanza tofauti ya pointi tano wote wamecheza mechi 26.
Kwenye mchezo uliowakutanisha watani hao wa jadi ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-0 Yanga huku watupiaji kwa Simba wakiwa ni Henock Inonga na Kibu Dennis.
Juma Mgunda, Kocha Msaidizi wa Simba amesema wanatambua kuna kazi ngumu ya kufanya kwenye mechi ambazo zimebaki lakini wapo tayari kushinda na inawezekana.
“Kuna malengo ambayo tunayo tukiwa ni timu na ukiagalia kwenye suala la ubingwa bado tupo kwenye mstari wa kupambania ubingwa kwa kuwa ligi haijaisha.
“Ikiwa tupo kwenye mbio za kuwania ubingwa hakuna ambaye amekata tamaa, inajulikana kuwa haijafika mwisho mpaka ifike mwisho.”
Post a Comment