Simba watambulisha kifaa kipya


 Klabu ya Simba SC leo Mei 25, 2023, imemteua Raia wa Uholanzi Mels Daalder kuwa Skauti Mkuu wa timu.


Mels ameshiriki kozi mbalimbali za scouting duniani ikiwa ni pamoja na kozi zinazoendeshwa na Skauti wa zamani wa Manchester United, David Hobson.


Mels ambaye ameshawahi kuishi Tanzania, ni shabiki mkubwa wa Simba pia ni mjuzi wa kufanya upembuzi (analysis) na ana ujuzi na ufahamu mkubwa wa Ligi ya Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika.


Mels anaongea lugha kadhaa ikiwemo, Kiholanzi, Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswahili kwa kiasi fulani.


Akizungumzia uteuzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Iman Kujula amesema; "Tuna furaha kubwa kumkaribisha Mels ili kuja kuboresha ufanisi kwenye scouting kwani ni eneo muhimu sana kwenye mafanikio ya klabu yetu. Tunaendelea na maboresho muhimu kuelekea msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa."

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post