Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Simba inatarajiwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja kiungo mshambuliaji Hassan Dilunga, imefahamika
Dilunga amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi 12 akisumbuliwa na majeraha, sasa yuko tayari kurejea uwanjani baada ya kupona
Miezi kadhaa nyuma Dilunga alijumuishwa kwenye kambi ya Simba akifanya mazoezi na timu ili benchi la ufundi liweze kumfanyia tathmini
Wakati Simba ikiwa kwenye mchakato wa kumsajili, imeelezwa JKT Tanzania iliyopanda ligi kuu msimu huu, nayo imeonyesha nia ya kutaka kumsajili
Hata hivyo habari za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Simba zimebainisha kuwa Kocha Robertinho Oliveira ameidhinisha Dilunga kusajiliwa na atapewa mkataba wa mwaka
Post a Comment