Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Serikali imethibitisha kifo cha shabiki mmoja wa Yanga SC kufuatia vurugu zilizozuka mapema nje ya uwanja huo wakati wa zoezi la mashabiki kuingia uwanjani
Taarifa ya awali iliyotolewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu imeeleza kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imepokea jumla ya majeruhi 30 ambapo mmoja amefariki (Mwanaume mwenye umri wa takribani miaka 40. ) na Majeruhi wengine wanaendelea vizuri baada ya kupata majeraha mbalimbali
Vurugu zilizuka nje ya Dimba la Benjamin Mkapa wakati mashabiki hao walipolazimisha kuingia ndani ya uwanja huo kabla ya milango ya uwanja huo kufunguliwa
Mashabiki hao walifika kushuhudia mchezo wa kwanza fainali ya kombe la shirikisho Afrika kati ya Yanga SC dhidi USM Alger
Post a Comment