Shabiki Simba awavaa Robertinho, Mgunda

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Shabiki maarufu wa Simba, Yusuph Mwenda ameonyesha kuchukizwa na kitendo cha kocha wa timu hiyo, Robertinho kupanga kikosi cha pili katika mechi yao dhidi ya Namungo hali iliyosababisha kutoa sare.


Mwenda aliyasema hayo wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa Ligi katika Dimba la Majaliwa.


"Sisi Simba hatutaki kujaribu kwenye mechi zetu, tungeshinda kwa Namungo jana tulikuwa tunawapa pressure Yanga wakiteleza tunakaa. Sasa makocha na viongozi walituaminisha vipi kwamba ubingwa bado tunaupambania.


"Kocha Mgunda anarahisha tu kuongea lakini tunaoumia ni sisi, yeye pale analipwa mshahara na posho tu, ila wenye timu ni sisi. Wameanzisha wachezaji ambao hawawezi kutusaidia kushinda," amesema Mwenda.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post