Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika juhudi za hamasa kuendelea kuunga mkono michezo nchini hususani katika mashindano ya kimataifa, imeamua kugharamia jumla ya mashabiki 55 watakaosafiri kuelekea nchini Afrika Kusini, kwenda kuishangilia klabu ya Yanga katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants, utakaopigwa tarehe 17 Mei, 2023 kwenye uwanja wa Royal Bafokeng uliopo katika mji wa Rustenburg nchini humo.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Said Yakubu alipokuwa anazungumza na vyombo vya habari leo tarehe 13 Mei 2023, katika ukumbi wa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa msafara huo wa hamasa utaongozwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Hamis Mwinjuma.
"katika hii safari, Serikali imesaidia Yanga kupeleka baadhi ya mashabiki 55 ambao wataondoka kesho jumapili tarehe 14 Mei, 2023 kueleka Afrika Kusini na huko wataungana na Watanzania waishio Afrika Kusini katika kuhakikisha wanatoa hamasa ya kutosha,na nimeongea na Balozi, wao pia wamejiandaa kuwapokea lakini pia wameandaa mabasi kutoka kila mji kuhakikisha Watanzania wanakuwa wengi katika mchezo huo,"amesema Yakubu.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa klabu ya Yanga, Andrew Ntime amesema kuwa wao kama timu wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mchezo huo huku akiishukuru serikali kutokana na mchango wake wa kupeleka mashabiki hao.
Post a Comment