Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Rais wa Jamhuri wa ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itatoa ndege binafsi kwa ajili ya kuisafirisha Timu ya Yanga itakapokwenda kucheza mchezo wake wa Fainali nchini Algeria dhidi ya USM Algier.
Yanga ambao wamefuzu hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika wataanzia nyumbani Mei 28 kisha watakwenda kumalizia Fainali ya Pili June 3 katika Uwanja Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa minara 21 ya kurushia matangazo ya televisheni ardhini (DTT) ya kampuni ya Azam Media ambapo alikuwa Mgeni rasmi Rais Samia amesema;
"Kama Serikali tutaoa ndege maalum ambayo itawapeleka katika mchezo wa Fainali, sasa ndege hiyo itabeba wachezaji, Mashabiki lengo ni kuwapa hamasa ili wakafanye vyema katika mchezo huo"
"Niwaombe viongozi wa TFF kuwapa moyo ili Kombe lije nyumbani na kuliletea sifa Taifa"
Post a Comment