Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally ameandika kwenye ukurasa wa Instagram ujumbe mzito kuhusu wachezaji makinda, Pape Sakho na Peter Banda.
Ahmed ameweka picha ya wawili hao na kuandika hivi:
Kuna wakati msimu uliopita Combination ya Sakho na Banda ilikubali sana, tukaaamini msimu huu wangefanya balaaa kubwaa lakini bahati mbaya haikua hivyo
Zipo sababu nyingi zilizopolekea makali yao kupungua lakini kubwa kabisa ni majeruhi ya wawili hao
Sakho aliumia na kukaa nje kwa muda mrefu na Banda aliumia na kukaa nje kwa zaidi ya miezi miwili
Tunaenda kuanza msimu mpya, Msimu wa tatu kwa Peter Banda na msimu wa tatu kwa Pape Sakho
Huu ndo msimu wa kula matunda ya vipaji kutoka Afrika ni muda wa Wonder Kids kuthibitisha ubora
Mungu awalinde vijana wetu dhidi ya Majeruhi.
Post a Comment