Robertinho amtaka mchezaji huyu wa Azam fc

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho' yupo siriazi kwelikweli akimtaja kiungo mkabaji na nahodha wa Azam, Sospeter Bajana baada ya kusisitiza kwa kuwaambia mabosi wa klabu


hiyo kuhakikisha wanamleta mkali huyo kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao.


Kiungo huyo ni mmoja ya wachezaji ambao wamependekezwa na kocha huyo raia wa Brazili kwa ajili ya kikosi cha msimu ujao ambacho amepanga kiwe moto kuliko cha msimu huu ambacho kimemaliza msimu kikiwa mikono mitupu bila kutwaa taji la aina yoyote ikiwamo Ligi Kuu, ASFC na kimataifa.


Bajana anayemaliza mkataba na klabu ya Azam amekuwa akitajwa ni chaguo la kwanza la Robertinho eneo la kiungo chja ukabaji na jana alisema kuwa, anahitaji wachezaji watakaoiongezea Simba nguvu kwa msimu ujao ili kufanikisha malengo yao kwa michuano ya ndani na kimataifa.


Robertinho aliyeajiriwa Simba katikati ya msimu huu akitokea Vipers ya Uganda akichukua nafasi ya Zoran Maki, ameshindwa kuvuka robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukwamishwa na kipigo cha penalti kutoka kwa watetezi wa taji hilo, Wydad ya Morocco iliyopo fainali kwa sasa dhidi ya Al Ahly ya Misri kutokana na timu hizo kupenya mbele ya Esperance na Mamelodi Sundowns.


Katika kuhakikisha anaanza msimu mpya akiwa moto, kocha huyo alisema anataka kuijenga Simba ambayo itakuwa bora zaidi 'haitashikika', hivyo ni muhimu akaongeza watu wataoipa nguvu moja kwa moja kwenye kila eneo elekezi ndani ya kikosi hicho kijacho na kwamba mmoja ni Bajana.


"Kazi iliyopo ni kumaliza vizuri msimu, haukuwa msimu wetu lakini jambo ambalo mashabiki wetu wanapaswa kutambua ni kwamba msimu ujao utakuwa tofauti mno, tupo kwenye mchakato wa kuendelea kujenga timu imara na bora zaidi, yaliyotokea hayaweza kuturudisha nyuma, hata kidogo,"


"Natamani kuona tukiwa na kila mchezaji ambaye tumeona na kujiridhisha naye kuwa anaweza kuongeza nguvu, baada ya msimu kumalizika nadhani ndio mambo mengine yatachukua zaidi nafasi kwa ukubwa zaidi lakini nipo na matumaini kuwa kila kitu kitaenda sawa," alisema kocha huyo, aliyeongeza kwa kusema kwa sasa analipanga jeshi lake ili kumaliza vyema mechi za Ligi Kuu Bara.


Simba itakwaruzana na Polisi keshokutwa kabla ya kuisubiri Coastal Union Juni 9 mechi zote zikipigwa jijini Dar es Salaam na kocha huyo alisema kazi ni ile ile ya kukusanya pointi tatu kama ilivyofanywa kwa Yanga na Ruvu Shooting aliyoishusha daraja wiki iliyopita kwa kuilaza mabao 3-0.


"Ni mechi ngumu kutokana na wenzetu kuwa kwenye hatari ya kushuka daraja, tutapambana kwa ajili ya kumaliza vizuri msimu na jambo zuri ni kwamba nitaendelea kutoa nafasi kwa mchezaji yeyote atakayekuwa tayari kimchezo, ili kuona tunazoa pointi zote sita kupitia mechi hizo mbili," alisema.


Rekodi zinaonyesha katika michezo mitano iliyopita baina ya timu hizo za Simba na Polisi, mnyama ameshinda mechi nne na moja iliisha kwa sare na maafande hao wanaoshika nafasi ya pili kutoka mkiani wakiwa na pointi 25 wanahitaji ushindi ili kuepuka kuifuata Ruvu au kucheza play-off.


MSIKIE BAJANA


Kwa upande wa Bajana alisema fikra na mawazo yake ni kuisaidia Azam kutimiza malengo ambayo walijiwekea, ikumbukwe kuwa matajiri hao wa Chamazi walitinga fainali ya ASFC baada ya kuifunga Simba kwa mabao 2-1.


"Nipo na jambo moja tu kichwani kwangu kwa sasa ambalo ni kufanikisha malengo ya timu," alisema mchezaji huyo na kusema hizo taarifa za kutakiwa Msimbzi anazisikia mitandaoni, ila muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi, ila kwa sasa yeye ni mchezaji wa Azam na ana kazi ya kumalizia vema msimu.


Azam iliyopo nafasi ya tatu kwa sasa ikiwa na pointi 54 baada ya mechi 28, huku ikiwa na tiketi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao licha ya kuwa na fainali ya Kombe la ASFC.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post