Rio Ferdinand amchana Carlo Ancelotti

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mchambuzi wa soka wa kituo cha televisheni BT, Rio ameshangwazwa na kitendo cha Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti kutompanga Antonio Rudiger, badala yake akamchezesha Eder Militao katika mechi ya marudiano ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Machester City.

Rudiger alicheza kwa kiwango bora katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, Militao alipoondolewa kikosini kutokana na kutumikia adhabu, Madrid ikalazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Man City.

Katika mchezo huo wa kwanza Rudiger alimzuia aika Erling Haaland asilete madhara Rio akashangazwa Rudiger alivyoachwa nje kikosi cha kwanza katika mechi ya marudiano juzi Jumatano (Mei 17).

Alipoulizwa kuhusu mabadiliko hayo aliyofanya Ancelotti, Rio aliiambia BT Sport: “Hata sielewi kwa nini Rudiger aliachwa benchi, wakati mwingine unafikiria hivi tumeshashuhudia beki ambaye angemzuia Haaland?

“Inashangaza kwakweli, kama Rudiger ana takwimu bora basi angeendelea naye tu, Ancelotti alikuja na kitu ambacho anakiamini, Rudiger alikuwa na kiwango bora tangu msimu uliopita, aliwasaida sana, unawezaje kumuacha benchi mtu ambaye ni mhimili wa timu,?

“Huwezi kataa Militao ni chuguo namba moja kikosini, je alikuwa na mchango zaidi msimu wote huu? Kama ningekuwa mimi ningefikiria zaidi kwa kilichotokea Ancelotti kazingua.”

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post