Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga kwa ushindi walioupata dhidi ya Timu ya Marumo Gallants na kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Sasa katika kuwapa hamasa Timu ya Yanga Rais Samia amesema atanunua kila goli kwa Tsh Milioni 20 iwapo wataibuka na ushindi katika michezo ya Fainali.
Akizungumza leo Alhamis katika hafla ya uzinduzi wa minara 21 ya kurushia matangazo ya televisheni ardhini (DTT), Rais Samia amesema;
"Tunapokwenda kwenye Fainali, ni miloni 20 kwa kila goli Timu inapotoka na ushindi sio ile wamefungwa mbili halafu wao wakafunga moja hapana"
Rais Samia aliahidi kuniunua kila goli kwa milioni 5 michezo ya Hatua ya makundi, Milioni 10 kwa kila goli hatua ya Robo Fainali na Nusu Fainali na sasa hatua ya Fainali imeahidiwa milioni 20 kwa kila goli timu inapoibuka na ushindi.
Post a Comment