Rais Samia awapongeza yanga kwa kutinga Nusu fainali "mmetuheshimisha"

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameipongeza klabu ya Yanga SC kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.


Yanga walifuzu hatua hiyo juzi Jumapili baada ya kutoka 0-0 na Rivers United ya Nigeria na kufanikiwa kufuzu kwa agrigatte kwani mchezo wa Robo Fainali ya awali nchini Nigeria, Yanga alishinda kwa 2-0.


Kupitia mitandao yake ya kijamii, Rais Samii ameweka pongezi zake kwa Yanga na kuwataka wafanye vizuri zaidi katika hatua zinazofuata.


"Pongezi kwa Klabu ya Yanga kwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup), na kila la kheri katika maandalizi mliyoanza sasa kwa mchezo ujao. Mmeandika historia jalili. Mmetuheshimisha sana. Hamasa yangu inaendelea, na sasa imeongezeka. Kaifanyeni kazi."

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post