Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza klabu ya Yanga SC kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
“Hongereni Yanga kwa ushindi katika mchezo wenu wa raundi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup)”.
“Nawatakia maandalizi mema kwa mchezo wenu wa raundi ya pili, muendelee kuiheshimisha nchi yetu. Hamasa yangu inaendelea,” amesema Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Mabao ya Yanga jana yalifungwa na viungo, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 64 na Mghana Bernard Morrison dakika ya 90 na ushei na sasa wanatakiwa kwenda kuulinda ushindi huo kwenye mchezo wa marudiano Mei 17 Uwanja wa Royal Bafokeng, Phokeng, NW.
Wakiitoa Marumo, Yanga watakutana na mshindi wa jumla kati ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast na USM Alger ya Algeria katika Fainali zitakazopigwa Mei 28 na Juni 3.
Post a Comment