Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ameitumia salamu za pongezi klabu ya Yanga kwa kuingia Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
“Pongezi za dhati kwa Klabu ya Yanga kwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup). Mmeandika historia na kuipa nchi yetu heshima kubwa sana. Nawatakia kila la kheri katika mchezo wenu wa Fainali,” amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Tayari Yanga imevuna jumla ya Sh. Milioni 40 katika mfuko wa hamasa wa Rais Samia kutokana na mabao manne waliyofunga kwenye mechi mbili za Nusu Fainali dhidi ya Marumo Gallants.
Yanga imeitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini jana na kwenye Fainali itakutana na USM Alger iliyoitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya sare ya 0-0 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani.
Yanga itaanzia nyumbani katika Fainali ya kwanza Mei 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Algeria kwa mchezo wa marudiano Juni 3 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers.
Post a Comment