Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wakati shauri la Kiungo wa Yanga Feisal Salum "Fei toto" likigonga mwamba kwa mara nyingine mbele ya Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji na kutambuliwa kisheria kuwa ni mchezaji wa Yanga.
Hatimaye mdau wa Soka na Mwenyekiti wa zamani w Klabu ya Simba SC, Alhaji Ismail Aden Rage ameonekana kukerwa na namna mchezaji huyo anavyokosekana uwanjani na kusisitiza kuwa anapoteza kipaji chake na Rage ametoa njia kwa mara nyingine ya namna ya kulitatua tatzo la mchezaji huyo baina yake na Klabu ya Yanga.
Akizungumza Rage amesema;
"Bahati mbaya watu wanaomzunguka Feisal Salum wanandanganya lakini kama Feisal Salum timamu ,mimi leo namshauri kama mzee wake ninayezijua Sheria za FIFA vizuri,kwamba Klabu inayomtaka isiogope ,iende ikaongee na Yanga kuwaeleza wanataka kuvunja Mkataba wa Feisal Salum, waelewane na hakuna kinachoshindikana,kama inawezekana Feisal aje anione mimi nitamsaidia,niwe kati kati,nitaongea na hiyo Klabu na pia Yanga,ni kazi ya saa chache tu na uzuri Yanga wao wapo wazi wamesema wapo tayari,sasa nashangaa kwanini hawaendi?
Feisal yuko nje ya Uwanja tangu Disemaba mwaka jana alipowasilisha barua ya kuomba kuvunja Mkataba Yanga, lakini ombi hilo lilipingwa na Klabu ya Yanga na kudai kuwa ni kinyume na taratibu.
Japokuwa mchezaji huyo aliitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa walipocheza dhidi ya Uganda michezo ya kuwania kufuzu AFCON.
Post a Comment