Novatus Dosmas anukia EPL

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail, Timu ya Southampton na Middlesbrough wameonesha nia ya kumsajili Novatus Dismas Miroshi kutoka klabu ya Zulte Waregem ya Ubelgiji.


Novatus mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Zulte msimu uliopita kutoka nchini Israeli, lakini ameendelea kuvutia kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi uwanjani.


Msimu huu Novatus amecheza kama kiungo, beki wa kushoto na wakati mwingine beki wa kati kwenye mfumo wa back three.


Licha ya timu yake kushuka daraja bado Miroshi ameendelea kuvivutia vilabu vikubwa.


Msimu huu Novatus amecheza michezo 36 akiwa na Zulte Waregem na kutoa pasi mbili za magoli huku akiichezea Taifa Stars na kufunga mabao mawili.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post