Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wananchi wana dakika 180 za kuwania ubingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya ushindi wa jumla wa mabao 4-1 dhidi ya Marumo Gallants katika mchezo wa nusu fainali
Jana Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Marumo katika mchezo wa nusu fainali mkondo wa pili uliopigwa Afrika Kusini huku pia ikishinda mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa wiki iliyopita
Yanga itachuana na USM Alger (USMA) katika hatua ya fainali baada ya Waarabu hao kutoka Algeria kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya ASEC Mimosas katika mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali uliopigwa huko Algeria
Timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa nusu fainali mkondo wa kwanza huko Ivory Coast
Fainali hii itakuwa kisasi kwa Yanga, Wananchi wakiwa na kumbukumbu ya timu hizo kukutana kwenye michuano hii hatua ya makundi mwaka 2018
USMA waliifunga Yanga 4-0 katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi uliopigwa Algeria na Yanga kushinda 2-1 katika mchezo wa marudiano
Wakati huo Yanga ilikuwa ikinolewa na kocha Mwinyi Zahera aliyetua kuchukua nafasi ya George Lwandamina ambaye alirejea kunako klabu yake ya zamani Zesco United
Mchezo wa fainali mkondo wa kwanza utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa May 28 na marudiano kupigwa Algeria Juni 03
Post a Comment