Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Salim Abdallah 'Try Again' amesema mshambuliaji Cesor Lobi Manzoki atakuja kuitumikia Simba pale mkataba wake utakapomalizika huko China
Hivi karibuni Try Again alithibitisha Simba kumsainisha mkataba wa awali Manzoki wakati akiwa na Vipers Fc kabla ya mchezaji huyo kutimkia Uchina baada ya kupata ofa nono zaidi
Try Again alisema Simba ilifanya kila jitihada kumsajili mchezaji huyo lakini hawakuwa na namna baada ya ofa kubwa kutoka China
Manzoki alikuja kwenye uchaguzi wa klabu ya Simba ambapo Try Again alibainisha kuwa alifanya hivyo kwa mapenzi yake mwenyewe na aligharamia safari yake mwenyewe
"Manzoki ni mchezaji mwenye mapenzi makubwa na Simba. Kama uongozi tulifanya kila linalowezekana ili tuwe nae hapa lakini ofa kutoka China ilikuwa nono zaidi. "
"Juzi tu nimeongea nae, nafikiri mkataba wake ukiisha anaweza kuja kucheza Simba," alisema Try Again
Aidha Try Again amesema wamejipanga kusajili kitaalam kuhakikisha hawarudii makosa yaliyojitokeza nyuma
"Ni kweli msimu huu haukuwa mzuri kwetu lakini niseme tutarekebisha. Tutasajili, tutasajili kitaalam, tutahakikisha tunapata wachezaji ambao watakidhi malengo na matamanio ya walio wengi"
Post a Comment