Mgunda: Hawa ndio wachezaji wa Simba, wote mmeona walivyocheza

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mgunda amesema kuwa kiwango walichokionyesha wachezaji wa Simba katika mchezo wa jana dhidi ya Namungo wamekiona na watakwenda kukifanyia kazi huku akiwasihi mashabiki wa klabu hiyo kuwavumilia wakati benchi la ufundi likifanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo huo.


Mgunda amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutamatika huku Simba akitoa sare ya bao 1-1 na Namungo katika Dimba la Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.


Simba ilichezesha wachezaji saba wa kikosi cha pili huku ikiwapumzisha nyota wake kadhaa wakiwemo Chsama, Tshabalala, Inonga, Kapombe, Mzamiru, Kibu Denis na Kanoute.


“Tumecheza na timu ambaypo wakiwa kwao wanakuwa bora sana, tumekuja kucheza kwa tahadhari lakini mapungufu yaliyojitokeza ndiyo yamesababisha tukapata sare. Hii ni sehemu ya mchezo, tunajipanga na mchezo ujao.


“Wachezaji wote waliocheza leo hakuna ambaye tumemleta kwa mkopo, wote ni wachezaji wa Simba na wamesajiliwa kuitumikia Simba, kwa hiyo ilikuwa sehemu yao kuitumikia Simba, kwa hiyo sioni ajabu wametimiza wajibu wao.


“Tumewapa nafasi ya kuitumikia klabu, tulichokiona ni cha kwetu, na mwenye macho yake ameona, hivyo tulichokusudia kukiona na Robertinho tumekiona, tutaenda kufanyia kazi mapungufu kwenye mechi zilizosalia.


“Tuwaheshimu wachezaji wetu wakipewa nafasi ya kuitumikia Simba, ni haki yao. Na hawa ndio wachezaji wetu tuliosajili Simba, kwa hiyo tuwe na imani nao. Kuhusu ubingwa siku zote nasema haiwi mwisho mpaka ifike mwisho,” amesema Mgunda.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post