Messi aomba msamaha Psg

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Siku ya Jumatano klabu ya PSG ilitangaza kumfungia Mshambuliaji wake raia wa Argentina Lionel Messi kwa muda wa wiki mbili.


Messi alifungiwa kutokana na tatizo la utovu wa nidhamu ambapo alisafiri kwenda Saudi Arabia bila ruhusa ya timu yake. Mbali ya kufungiwa taarifa za ndani zinaeleza kuwa atakatwa mshahara wake pia.


Messi ameomba msamaha klabu yake ya PSG pamoja na wachezaji wenzake ambapo ameeleza kuwa safari ile ilikuwa ya muhimu sana na ilikuwa ngumu kusitisha kwani alishawahi kusitisha mwanzo na mara hii kila kitu kilikuwa kimepangwa na alikuwa anasubiriwa yeye.


Watu wa karibu ya Messi wameeleza kuwa Messi anatarajia kuondoka mwishoni mwa msimu huku klabu za Al Hilal ya Saudi Arabia na Barcelona zikitajwa kuwa huenda Messi akajiunga nazo mmoja wapo.


Baada ya taarifa hiyo Mashabiki wa PSG walijawa na hasira na kuamua kuandamana hadi uwanjani na kumtaka Messi aondoke.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post