Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amesema anajivunia kuhusika kwenye mafanikio ya timu yake ya Yanga katika michuano mbalimbali, huku akikiri kuwa huu ndio msimu bora zaidi kwake katika maisha yake ya soka
Akizungumza baada ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Singida Big Stars na Yanga uliopigwa jana mkoani Singida na yeye kufunga bao pekee katika mchezo huo, hivyo kuipeleka Yanga hatua ya fainali, amesema msimu huu umekuwa wa mafanikio kwake katika michuano ya kitaifa na kimataifa
"Nmeshiriki michuano ya CAF mara nyingi lakini sikuwahi kufunga mabao saba au sita, nilikuwa ninafunga, lakini mabao matatu au mawili kwa hiyo nina furaha sana na msimu huu," alisema Mayele
Mayele anaongoza katika ufungaji Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 16, lakini pia ana mabao sita katika Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Yanga imeingia hatua ya fainali
Katika msimu huu Mayele amfunga mabao 33 katika mashindano yote
Post a Comment