Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mchezo wa mkondo wa kwanza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo umemalizika kwa wageni USM Alger kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
Mabao ya USM Alger yalifungwa na Mahious kwenye dakika ya 32 na Merili katika dakika ya 86 ikiwa ni dakika mbili baada ya Fiston Mayele kuifungia Yanga bao la kusawazisha
Yanga ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi lakini haikuwa rahisi kuipenya ngome ya USM Alger waliokuwa wakicheza kwa kujihami zaidi huku wakishambulia kwa kushitukiza
Mvua inayoendelea kunyesha jijini Dar es salaam ni kama ilipunguza radha ya mchezo ambao ulishuhudiwa na mashabiki 60,000
Yanga ina dakika nyingine 90 za kupambana ugenini ambao Wananchi watahitaji kushinda kwa angalau mabao mawili ili waweze kuwa mabingwa
Post a Comment