Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mchezo wa ligi kuu kati ya Namungo Fc dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa Majaliwa, umemalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1
Jean Baleke aliendeleza kasi yake ya kutupia mabao kwenye ligi akiitanguliza Simba kwa bao safi kwenye dakika ya 28 kabla ya Hassan Kabunda kuisawazishia Namungo Fc kwenye dakika ya 39
Ulikuwa mchezo ambao mabadiliko makubwa ya kikosi cha kwanza cha Simba yaliathirithi ufanisi wa wekundu wa Msimbazi ambao Kocha Robertinho Oliveira aliweka nyota wengi nje akisubiri mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam Fc siku ya Jumapili
Simba imefikisha alama 64 ikiendelea kusalia nafasi ya pili kwa tofauti ya alama nne dhidi ya Yanga ambayo kesho itacheza na Singida BS
Post a Comment