Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Msaidizi wa Simba Juma Mgunda amesema anatambua maumivu ambayo Wanasimba wanapitia baada ya kushuhudia timu yao ikitokewa hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa kufungwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa jana uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara
Mgunda amesema matokeo hayo yamewaumiza hata wao katika benchi la ufundi, watajipanga na kufanya tathmini ya kilichotokea msimu huu ili kujipanga na kufanya vizuri zaidi msimu ujao
"Mimi naijua nguvu ya mashabiki uwanjani, ndio maana wanasema ni mchezaji wa 12, matokeo haya yamewaumiza sana lakini hata sisi benchi la ufundi tumeumia kwani halikuwa kusudio letu. Mtu wa kwanza ambaye anataka matokeo ya ushindi ni Kocha na benchi lake la ufundi"
"Inapotokea matokeo ya namna hii yanaumiza, niwaambie mashabiki wa Simba kwamba imetuumiza sote. Kikubwa ni kujipanga na kukaa chini kuangalia tulikosea wapi ili siku za mbeleni tuweze kufanya vizuri zaidi"
"Naweza kusema msimu huu haujawa mzuri kwetu lakini sisi benchi la ufundi tumeona, viongozi wa Simba wameona na hii ni taasisi kubwa, itachukua hatua kurekebisha mapungufu ili kuhakikisha msimu ujao tunafanya vizuri," alisema Mgunda
Baada ya kipigo cha Azam Fc, ni kama Simba imepoteza matumaini ya kushinda taji lolote msimu huu kwani wako nyuma kwa alama saba kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC huku zikiwa zimesalia mechi tatu tu
Post a Comment