Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Historia inakwenda kuandikwa uwanja wa Benjamin Mkapa leo ambapo utashuhudiwa mchezo wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Marumo Gallants
Ni kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Benjamin Mkapa timu ya Tanzania itacheza mechi ya nusu fainali katika mashindano ya CAF ngazi ya klabu
Utakuwa mchezo muhimu kwa Yanga kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga fainali wakati timu hizo zitakaporudiana wiki ijayo huko Afrika Kusini
Kwa mashabiki wa soka nchini hii ni fursa adimu, kushuhudia mchezo wa nusu fainali mashindano ya CAF katika ardhi ya Tanzania
Kwa wale ambao bado hawajapata tiketi wanayo nafasi ya kununua tiketi kwani bado mauzo ya tiketi hayajafungwa
Tiketi za VIP A zimemalizika hivyo tiketi zinazopatikana ni VIP B, C na Mzunguuko
Jana wakati anazungumza na Wanahabari, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi aliwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao
Nabi alisema nguvu ya mashabiki iliwasaidia kufanya vizuri katika mechi zote walizocheza nyumbani katika mashindano hayo msimu huu sasa wanawahitaji kwa wingi zaidi leo katika mechi muhimu ya kusaka tiketi ya kutinga fainali
Alibainisha kuwa wachezaji wake wote wako tayari kwa mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 10 jioniPia mechi itakuwa LIVE kwenye app yetu bofya hapa kuidownload sasa
Post a Comment