Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa ambapo mkoani Singida walima alizeti wa Singida BS watakuwa uwanja wao wa nyumbani LITI kuchuana na mabingwa watetezi Yanga
Singida BS wako katika vita ya kuwania nafasi ya tatu hivyo ni wazi watazihitaji alama zote tatu mbele ya Yanga ili kurejea nafasi hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na Azam FC
Hata hivyo wanachuana na Yanga ambayo hesabu imeelekeza kwenye kutetea ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo
Kimahesabu Yanga inahitaji kushinda mechi mbili tu kati ya nne zilizosalia ili kutetea ubingwa
Kama Wananchi watashinda leo basi watakuwa na deni la alama tatu tu ili kutetea ubingwa wao na wanaweza kufanikisha hilo katika mchezo utakaofuata dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa dimba la Azam Complex, jijini Dar es salaam
Baada ya watani zao Simba kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo Fc jana, Yanga inaweza kunufaika na kuteleza huko kwa watani zao kama itashinda leo
Mchezo utapigwa saa 10 jioni katika uwanja wa LITI Mechi itakuwa LIVE kwenye app yetu bofya hapa kuidownload bure sasa
Post a Comment