Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Feisal ndio tunachanga kama ulivyotuomba lakini maswali ya baadhi ni kuwa kwanini tunachanga pesa? Majibu ni kuwa Feisal anataka kwenda CAS kushtaki ili avunje mkataba wake na Yanga kwakuwa TFF hawajamtendea haki na Yanga pia.
Lakini maswali yanarudi kwani si ni Yanga wamekuita sana uende Jangwani mkamalizane? Wao hawana shida na wewe kuondoka! Sasa kwanini huendi Jangwani? Ni swali hili.
CAS inahitajika Million 56, lakini Jangwani inahitajika nauli au mafuta tu ya kufika pale ili mmalizane kwa amani kwakuwa wapo tayari uende, sasa kwanini twende kwenye gharama wakati kuna njia nyepesi?
Tutachanga ifike hiko kiasi, kesi itaunguruma wakati ambao huchezi na bado watasema ulipe huenda ama kesi ikaenda tofauti huenda, hapo huoni muda unapotea bure?
Kama ambavyo sisi tunakupa ushirikiano wa kuchanga em tuambie kwanini hutaki njia rahisi ya kwenda Jangwani, kukaa nao chini na kuvunja mkataba mutually? Watazame thamani yako na muda uliosalia kisha ukaondoka kirahisi tu? Em tuambie Maestro kuna nini kinatia ugumu? Maana wao hawakutaka njia yako na sio sahihi kimpira, wanataka ufuate njia ya mpira sasa ni kosa?
Binafsi nimetoa BUKU MBILI kwakuwa ilikuwepo tu lakini bado nashangazwa na hii njia ndefu uliyoamua kuchukua! Nafikiri kuna namna ukatuliza kichwa vyema na kufanya maamuzi sahihi, unaelewa lakini kesi zilivyo kama hazina baraka ya TFF ama shirikisho la soka la nchi yako?
Ameandika Farhani Kihamu
Post a Comment