Mashtaka sita yanayomkabili staa Fei Toto dhidi ya Yanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Katika barua ambazo zimevuja iliyoelekezwa kwa Feisal, Mei 16 alipokea barua ya malalamiko kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo ikimtuhumu kwa makosa mbalimbali ya kinidhamu.


Barua hiyo pia ilimuelekeza Feisal kuhudhuria kikao cha kamati ya sheria na nidhamu kitakachosikiliza mashtaka dhidi yake mnamo tarehe 24 (juzi), Mei 2023 saa 4:00 asubuhi katika ofisi za klabu zilizopo Jangwani ukumbi wa mikutano.


Hati ya mashtaka yanayomkabili kiungo mshambuliaji wa Yanga Feisal  Salum.


UTORO KAZINI


Kwamba Feisal Salum Abdallah akiwa mwajiriwa na mchezaji wa Young Afrika Sport Club kwa Mkataba  wa Ajira unaoisha tarehe 30 Mei 2024 bila sababu yoyote ya msingi umekuwa mtoro kazini kwa kutokaa kambini tangu tarehe 22 Desemba, 2023 kinyume na kipengele cha 8.1.1 na 8.1.3 cha Mkataba wako wa ajira wa tarehe 10 Agosti, 2020 na kanuni na mwenendo wa Timu ya Yanga


MATUMIZI MABAYA YA LUGHA YENYE NIA YA KUSHUSHA HESHIMA YA KLABU


Kwamba Feisal Salum Abdallah akiwa mwajiriwa wa Young Africans Sports Club kwa Mkataba wa ajira unaoisha tarehe 30 Mei 2024 kwa nia ovu umekuwa ukitoa taarifa zisizo sahihi kwa umma ukieleza kuwa mwajiri wako anakunyanyasa huku ukijua kuwa taarifa hizi siyo za kweli na hivyo kuishushia Young Africans Sports Club heshima mbele ya umma, mashabiki na wapenzi wa soka kinyume na Kipengele cha 8.1.16 cha Mkataba wako wa ajira wa tarehe 10 Agosti, 2020 na kanuni za Mwenendo  wa Timu ya Yanga (Young Africans SC First Team Player Code of Conduct)


KUKATAA KUTII MAELEKEZO HALALI YA KLABU


Kwamba Feisal Salum Abdallah ukiwa mwajiriwa na mchezaji wa Young Africans Sports Club kwa Mkataba wa Ajira unaoisha tarehe 30 Mei, 2024 kwa makusudi  nia ovu ulikataa kutii maelekezo kwa ajili ya kuitumikia Klabu baada ya kuwa umetoka kambini bila sababu za msingi kinyume na Kipengele cha 8.1.6  cha Mkataba wako wa ajira wa tarehe 10 Agosti, 2020 na kanuni za Mwenendo wa Timu ya Yanga (Young Africans SC First Team Player Code of Conduct)


KUFANYA VITENDO VYA HUJUMA (SABOTAGE) DHIDI YA KLABU


Kwamba Feisal Salum Abdallah akiwa mwajiriwa na mchezaji wa Young Africans Sports Club kwa Mkataba wa ajira unaoisha tarehe 30 Mei, 2024 kwa makusudi na nia ovu ukijua kuwa Klabu ilikuwa katika mashindano muhimu ya kuwania ubingwa wa NBC Primier  League, CAF Confederation Cup na Azam Confederation Cup na umekuwa ukifanya hujuma kwa Klabu kwa kuwachonganisha wachezaji wazawa na wale wa kigeni kwa kutaka kuonyesha kuwa wachezaji wazawa wanaonewa na kwamba wewe unafanya hatua za kuwakomboa kitendo ambacho ni hatari kaa ustawi na umoja wa wachezaji wa Klabu kinyume na Kipengele cha 8.1.19 na 8.1.16 cha Mkataba wako wa ajira wa tarehe 10 Agosti, 2029 na kanuni za Mwenendo wa Timu ya Yanga (Young Africans SC First Team Player Code of conduct)


KUANZA MAZUNGUMZO NA KUHAMIA KLABU NYINGINE WAKATI MKATABA WAKO UKIWA HAI


Kwamba Feisal Salum Abdallah akiwa mwajiriwa na mchezaji wa Young Africans Sports Club kwa Mkataba wa ajira unaoisha tarehe 30 Mei, 2024 bila sababu ya msingi na kwa nia ya kuhama Klabu ya Young Africans Sports Club, ulianziasha mazungumzo la Klabu nyingine kwa maelezo kuwa huna "mahaba" tena na Klabu ya Young Africans Sports Club kinyume na Kipengele cha 8.1.18 cha Mkataba wako wa ajira wa tarehe 10 Agosti, 2020 na kanuni za Mwenendo wa Timu ya Yanga (Young Africans SC First Team Player Code of Conduct)


KUKATAA KUTII MAAMUZI YA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA


Kwamba Feisal Salum Abdallah akiwa mwajiriwa na mchezaji wa Young Africans Sports Club kwa Mkataba wa ajira unaoisha tarehe 30 Mei, 2024 bila sababu ya msingi ulikataa kutii maamuzi sahihi ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) yaliyokutaka kuendelea kutumikia ajira na yako na Young Africans Sports Club mpaka  mwisho wa Mkataba wako wa ajira kinyume na Kipengele cha 8.1.21 cha Mkataba wako wa ajira wa tarehe 10 Agosti, 2020.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post