Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Marumo Gallants kutoka ligi kuu ya Afrika Kusini wameshuka daraja baada ya kupoteza mchezo wao wa mwisho wa ligi Kuu dhidi ya Swallows kwa kufungwa Magoli 2-
Katika mchezo huo uliopigwa jana, Marumo walihitaji ushindi ili wafikishe alama 32 ambapo zingewaweka salama
Timu hiyo iliwashangaza wengi kwa kufanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika lakini safari yao ikaishia mikononi mwa Yanga kwa kuchabangwa jumla ya mabao 4-1 katika mechi zote mbili za nusu fainali
Marumo na Mameloi Sundowns zimeondoshwa katika mashindano ya CAF hatua ya nusu fainali
Mamelodi waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa waliondoshwa na Wydad Athletic kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 nyumbani
Mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Morocco ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Post a Comment