Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mlinda lango namba moja wa Simba na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Aishi Manula anatarajiwa kupelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kuumia akiwa kwenye majukumu na klabu yake
Manula aliumia kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Ihefu Fc, mchezo ambao Simba ilishinda mabao 5-0
Meneja wa Manula Jemedari Said amesema bado mchezaji huyo anauguza jeraha na klabu ya Simba inajiandaa kumpeleka Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi
"Mchezaji ni wa klabu kwa hiyo mwenye jukumu la kumtibu ni klabu yake ya Simba. Tayari taratibu zimeshafanyika na muda si mrefu atapelekwa kwenye matibabu wiki hii"
"Amepelekwa Muhimbili, ikaonekana kuna damu imevuja kwa ndani na madaktari wakabaini msuli umekatika kwa hiyo anahitaji upasuaji ambapo utafanyika nje ya nchi," alisema Jemedari
Post a Comment