Man City wamposti Toure kuondoa laana ya mizimu ya Afrika kwa Guardiola

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Club ya Manchester city ni kama wamekubali wayamalize na nyota wa zamani wa club hiyo Yaya Toure raia wa Ivory coast kufuatia laana inayosemekana kutoka kwake kupitia kwa manager wake aliyompa Mkufunzi wa timu hiyo Guardiola kutokushinda UEFA CHAMPIONS LEAGUE maisha yake yote.


Manager wa Yaya Toure Dmitri Seluk alidai kuwa Guardiola atapata laana kutoka kwa wazee wa kiafrika ya kutokushinda tena UEFA CHAMPIONS LEAGUE maisha yake yote baada ya kutothamini wachezaji wa kiafrika akiwemo mteja wake Yaya Toure.


Mashabiki wa soka duniani waliamimi uwepo wa laana hiyo baada ya Guardiola kushindwa kushinda UEFA tangu maneno hayo yaongeleke,manchester city msimu uliopita iliondolewa kwenye hatua ya nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Real Madrid licha ya kuwa na timu bora.


Siku ya jana Manchester city wameonyesha kutambua mchango wa Yaya Toure na kuchapisha video kwenye ukurasa wao wa Instagram masaa machache kabla ya kuwavaa Real Madrid kwenye nusu fainali ya Uefa champions league.


Watu wengi wametafsiri pengine wameamua kuyamaliza na Yaya Toure ili msimu huu walau Guardiola achukue kombe hilo ambalo hajawahi kuchukua Tangu laana hiyo iwekwe.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post