Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ligi Kuu ya NBC inaelekea mwisho ambapo leo mchezo mmoja wa kiporo kati ya Namungo Fc dhidi ya Simba itapigwa katika uwanja wa Majaliwa, Ruangwa
Ni mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na kila timu kuwa na malengo tofauti
Wenyeji Namungo Fc wanawania kumaliza katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi ili kuvuna mamilioni ya wadhamini Azam Media wakati Simba bado iko kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu
Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, Simba imebaki na mashindano mawili ya ndani ambayo ni Ligi Kuu na FA
Ushindi katika mchezo dhidi ya Namungo leo utawafanya wapunguze gap la pointi dhidi ya watani zao Yanga kuwa mbili kabla ya mchezo wa Singida BS dhidi ya Yanga ambao utapigwa huko Singida Alhamisi
Baada ya mchezo huo, Simba itaelekea Mtwara inakokabiliwa na mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Jumapili, May 07
Mchezo kati ya Namungo dhidi ya Simba leo utapigwa saa 1 usiku Mechi itakuwa live kwenye App yetu bofya hapa kuidownload sasa
Post a Comment