Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze raia wa Burundi amesema kuwa tayari wameanza kuwafuatilia wachezaji na mbinu za wapinzani wao Marumo Gallants ya Afrika Kusini watakaokutana nao kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho ili kupanga mpango kazi wao wa kuwakabili na kupata matokeo.
Nabi amesema hayo wakati akihojiwa na Yanga TV mara tu baada ya mchezo huo war obo fainali ya Kombe la Shirikisho kumalizika katika Dimba la Mkapa.
“Ni furaha kubwa kwa wachezaji, wanachama, mashabiki na mpira wa Tanzania kuona kama kuna timu inaweza kufika nusu fainali. Kadri unavyosogea mbele ndipo unatamani kupata mafanikio zaidi, kwa sasa tuta concentrate na mechi zaijazo ili kuhakikisha tunapata tunachokitaka.
“Malumo Gallants itakuwa ni mchezo wenye ufundi mkubwa, ukiangalia ni timu ambayo haijatoka uwanjani bila kufunga bao, ni timu yenye wachezaji wanaocheza vizuri, wana kasi na mbinu kubwa, kwa hiyo utakuwa mchezo mzuri kwenye maeneo yote.
“Tunaamini tuna kikosi bora, kilichokomaa na kinachoweza kutupa kile tunachokitaka, tunaamini tutafanya kazi yetu vizuri ili kupata matokeo mazuri,” amesema Kaze.
Marumo Gallants inafundishwa na aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr ambaye anazijua vizuri timu za Tanzania na soka la Afrika kwa ujumla.
Post a Comment