Jordi Alba aaga FC Barcelona kwa kilio

 

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Beki wa pambeni wa FC Barcelona, Jordi Alba alimwaga chozi baada ya kuagwa katika Uwanja wa Camp Nou mwishoni mwa juma lililopita.


Alba aliagwa baada ya mechi ya mwisho ya msimu FC Barcelona ilipocheza dhidi ya Real Mallorca na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.


Beki huyo aliweka wazi ataondoka msimu utakapomalizika baada ya Sergio Busquets naye alipotangaza kwamba hatakipiga Barcelona msimu ujao.


Alba anaondoka Camp Nou kwa mara ya mwisho baada ya kufanyiwa mabadiliko dakika ya 79 dhidi ya Mallorca nafasi yake ikachukuliwa na Marco Alonso.


Beki huyo aliyechezea timu ya taifa ya Hispania mechi 91 alishindwa kujizuia na akaanza kulia huku akiwapungia makofi mashabiki.


Vilevile wachezaji wa Barcelona wakambeba juu Alba huku wakimrusha hewani kama ishara ya kumuaga kutokana na mchango wake kwenye klabu.


Wiki iliopita taarifa ziliripoti beki huyo mwenye umri wa miaka 34 ataondoka baada ya kudumu kwa muda wa miaka 11 Barcelona.


Ikaelezwa Alba ataondoka kutokana na kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake licha ya kubakisha mkataba wa mwaka mmoja. Baada ya tukio hilo Alba akawaaga mashabiki kupitia akaunti zake za mitando ya kijami.


Alba alijiunga na Barcelona akitokea Valencia kwa ada ya uhamisho wa Pauni 11 million mwaka 2012. Amefunga mabao 27 katika mechi 458 za La Liga akiwa na uzi wa Barcelona. Makombe aliyobeba La Liga sita, Copa del Reys na Ligi Mabingwa Ulaya.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post