Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Timu ya JKT Tanzania imefanikitwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa Mabao 7-2 dhidi ya Mkwawa Queens jana Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Wapinzani wao wakuu katika mbio za ubingwa na waliokuwa mabingwa pia, Simba Queens ambao jana wameshinda bao 1-0 dhidi Ceasiaa Queens Uwanja wa Chuo Kikuu cha Mkwawa mjini Iringa pia.
Kwa matokeo hayo, JKT Queens inamaliza na pointi 46, moja zaidi ya Simba Queens, wakati Fountain Gate Princess iliyomaliza na pointi 41 imeshika nafasi ya tatu na Yanga Princess yenye pointi 34 ni ya nne.
JKT Queens wanatwaa ubingwa bila kupoteza mechi yoyote (Unbeaten). Wamefikia rekodi ya Simba ya kuchukua kombe mara 3 ambapo wamebeba msimu wa 2017/18, 2018/19 na 2022/23
Post a Comment