Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mshambuliaji wa Simba SC, Jean Baleke amesema kuwa mara baada ya msimu kuelekea ukingoni na timu yao kushindwa kutwaa ubingwa wa ligi, hana budi kujipanga kwa ajili ya kuhakikisha kuwa msimu ujao unakuwa msimu mzuri kwao kwa kufunga mabao ya kutosha.
Baleke ambaye ni ingizo jipya ndani ya Simba SC mpaka sasa amekuwa mshambuliaji tegemeo ndani ya timu hiyo mara baada ya Moses Phiri kupatwa na majeraha ambayo yamemuweka nje kwa muda mrefu.
Baleke amesema kuwa: “Msimu ndio kama umeshaisha baada ya wenzetu kubebe ubingwa, kwa sasa tunapambana kuhakikisha kuwa michezo iliyobaki tunashinda na tunaanza maandalizi ya msimu ujao.
“Binafsi kwa msimu ujao malengo yangu ni kuhakikisha kuwa naipambania Simba kwa kufunga mabao mengi yatakayoiwezesha Simba kubeba ubingwa wa ligi kuu na katika michuano mingine ambao tutashiriki, msimu huu haujamalizika vizuri kwetu.
“Mashabiki wanatambua kuwa huu pia haukuwa msimu mzuri kwetu na kwao lakini tunawaahidi msimu ujao utakuwa ni msimu wa kitofauti zaidi kwani lazima tuwapatie mafanikio.”
Chanzo: Dar24
Post a Comment