Inshu nzima ya Bruno Gomes kutua Yanga imekaa hivi

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kiungo wa Singida BS, Bruno Gomez alizua gumzo zaidi jana baada ya kwenda kwenye benchi la Yanga na kuwasalimia wachezaji wa akiba pamoja na makocha wao kabla mchezo haujaanza.


Pia baada ya mchezo kumalizika alionekana akizungumza mara kwa mara na viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo, hali ambayo iliwafanya wengi waamini kuwa anaweza kujiunga na timu hiyo ya Jangwani mwishoni mwa msimu huu.


Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga ambazo tumethibitishiwa ni kwamba vigogo wa Yanga tayari wameshamalizana na kiungo Gomez.


Bruno ameonyesha uwezo mkubwa wa kucheza nafasi tofauti uwanjani kwa ufanisi wa hali ya juu ambapo hadi sasa ametumika kama namba sita, namba nane, namba 10 na pia winga huku akifanya vizuri katika ufungaji wa mabao na kupiga pasi za mwisho.


Fundi huyo wa upigaji mipira iliyokufa, hadi sasa ameifungia Singida Big Stars mabao tisa kwenye Ligi hadi sasa.


Hata hivyo, inadaiwa kwamba Yanga haitapata tabu kumnasa Bruno kwa kile kinachodaiwa uhusiano mzuri wa timu hizo.


Hivi karibuni, Singida Big Stars iliipa Yanga kipa Metacha Mnata kwa mkopo siku ya mwisho ya usajili baada ya kipa wa Wana Jangwani, Abou Mshery kuumia.


Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga imeondoka na alama tatu ugenini baada ya kuwachapa wenyeji wao Singida Big Stars kwa mabao 2-0 kwenye mchezo uliomalizika katika Uwanja wa CCM Liti Mkoani Singida

Chanzo: Mwanaspoti

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post