Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wachezaji Djigui Diarra na Khalid Aucho wataukosa mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Singida BS utakaopigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa LITI kutokana na sababu mbalimbali
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabri mapema leo, Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema Diarra alipata matatizo ya kifamilia wakati Aucho aliumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Marumo Gallants
"Wachezaji wako tayari isipokuwa mpaka sasa tuna uhakika wa kuwakosa Djigui Diarra na Khalid Aucho ambao wana changamoto ambazo ziko nje ya uwezo wetu"
"Tumekuwa na muda mfupi tangu mchezo uliopita dhidi ya Marumo Gallants, zaidi tumefanya recovery kuondoa uchovu na leo tutakamilisha mazoezi ya mwisho"
"Kiakili tuko vizuri, tunaheshimu mpinzani ambaye tutacheza nae tunataka kushinda ili tuingie fainali," alisema Kaze
Winga Denis Nkane amesema pamoja na kukosa muda wa kufanya mazoezi, wachezaji wako tayari na wanatambua umuhimu wa mchezo huo wakihitaji kushinda waweze kutinga fainali
Post a Comment