Coastal Union yaachana na Emery Nimubona

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Uongozi wa Wagosi wa Kaya ‘Coastal Union’ umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Beki wa kulia kutoka nchini Burundi Emery Nimubona.


Beki huyo alijiunga na Coatsla Union baada ya kuachana na Kayanza United FC ya nchini kwao Burundi na ni miongoni mwa wachezaji ambao waliaminiwa huenda wangeibeba Mangushi, kutokanana uzoefu alioao.


Nimubona ambaye aliwahi kuitumikia Simba SC, amethibitisha taarifa hizo huku akiweka wazi ni makubaliano ya pande mbili na hakuna mgongano wowote wa kimaslahi baina yake na viongozi wa Coastal Union.


“Kuna mambo mengine ambayo nisingependa kuyaweka wazi lakini ujue tu nimepewa barua ya kuachana nao hivyo sitokuwa tena sehemu ya kikosi cha Coastal Union kwa msimu ujao,” amesema Nimubona.


Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Coastal, Omary Ayoub amesema hakuna shida baina yao na Nimubona na kitendo cha kuachana ni cha kawaida kwani katika maisha ya mpira mambo hayo hutokea.


“Kila kitu tutakiweka wazi baada ya msimu kuisha kwa sababu sio yeye tu wapo wachezaji wengine ambao tutaachana nao na kusajili wapya tutakaoendana nao kama ilivyokuwa utaratibu,” amesema


Chanzo: Dar24

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post