Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Yanga imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuichapa Dodoma Jiji mabao 4-2 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Kennedy Musonda aliitanguliza Yanga kabla ya Dodoma Jiji kufunga mabao mawili kupitia kwa Collins Opare na Seif Karihe
Ilikuwa presha kuwa kwa Yanga baada ya kuwa nyuma kwa muda mwingi wa kipindi cha pili lakini wakatumia dakika 15 za mwisho kuonyesha kwa nini wametwaa ubingwa msimu huu
Mudathir Yahya aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Stephane Aziz Ki alikuwa shujaa wa Wananchi leo akifunga mabao mawili
Aliisawazishia Yanga bao la pili kabla ya Farid Mussa kufunga la tatu na Mudathir kuongeza la nne kwenye dakika za majeruhi
Alama 74 zimeihakikishia Yanga kutwaa ubingwa ikiwa na michezo miwili mkononi kwani Simba hata ikishinda mechi zilizosalia itafikisha alama 73
Post a Comment