Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said jana alialikwa kwenye kipindi cha Soccer Africa katika Makao Makuu ya DSTV huko Afrika Kusini
Ulikuwa mwendelezo wa mialiko ambayo Injinia Hersi alipata wakati yuko Afrika Kusini na kikosi cha Yanga kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants, Yanga ikifanikiwa kutinga fainali
Kabla ya mwaliko wa DSTV, Hersi alifanya mahojiwa na Robert Marawa wa 947 na Shirika la utangazaji la Afrika Kusini (SABC)
Mafanikio ya Yanga katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika msimu huu yamewashtua wengi, Hersi ametumia fursa hiyo kuitangaza vyema Yanga na nchi ya Tanzania
Post a Comment