Bado tuna dakika 90 Algeria - Kamwe

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewapongeza wanachama na mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao katika mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger


Mchezo huo umeweka rekodi ya kuhudhuriwa na mashabiki wengi kwani yawezekana walioingia uwanja leo ni zaidi ya 60,000


Pamoja na matokeo kutokuwa mazuri kwa Yanga, Kamwe amewataka Wananchi wasikate tamaa kwani bado kuna dakika nyingine 90


"Pongezi kubwa kwa Wanachama na mashabiki wetu kwa kuja kwa wingi ndani ya uwanja wa Mkapa. Historia imeandikwa Pengine huu ndio mchezo uliohudhuriwa na mashabiki wengi zaidi tangu uwanja wa Mkapa ulivyoanza kutumika"


"Tumepoteza mchezo lakini hizi ni Dakika 90 za kwanza. Bado 90 nyingine za kupambana kule Algeria. Rekodi yetu kwenye mechi za ugenini inatupa nguvu ya kuamini zaidi," alisema Kamwe


Baada ya kupoteza nyumbani kwa mabao 2-1 leo, Yanga itahitaji kufunga mabao mawili Algeria ili kuwa na nafasi ya kuwa mabingwa

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post