Alicho kisema kocha wa yanga baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya marumo gallants

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Marumo Gallants leo ni matokeo muhimu nyumbani lakini bado wana kazi ya kwenda kupambana kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Afrika Kusini wiki ijayo ili kuhakikisha wanatinga fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika


Nabi amesema jambo alilofurahia ni ushindi lakini hakuridhishwa na jinsi wachezaji wake walivyocheza hasa kipindi cha kwanza


Nabi amesema wachezaji wake hawakutumia nafasi nyingi walizotengeneza leo


"Wachezaji wangu hawakucheza vile namna nilitarajia wangecheza, tumepoteza nafasi nyingi lakini muhimu tumepata ushindi ambao tutakwenda nao kwenye mchezo wa marudiano tukifahamu tuna kazi ya kusaka matokeo mazuri ili tufuzu hatua inayofuata" alisema Nabi

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post