Ahmed Ally: Lazima tufanye usajili mpya

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Meneja wa Habari na Mawasiliano ya Simba SC Ahmed Ally, amesema kufika hatua ya Robo Fainali mara tatu haina maana klabu hiyo imefeli kwa sababu Mamelodi Sundowns inayosifiwa kwa ubora Afrika kwa misimu mitano imekuwa ikiishia Robo Fainali na sasa wamefanikiwa kutinga Nusu Fainali.


Simba SC kwa mara ya tatu imeshindwa kuvuka Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, pia imeshindwa kufanya hivyo katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani humo.


Ahmed ally amesema: “Kama Simba SC tumecheza Robo Fainali tatu tunaambiwa tumefeli vipi hao walicheza mara tano na msimu huu kufanikiwa, bado tuna sababu ya kujivunia kwa hapa tulipofikia na kusahihisha makosa yetu na kujifunza kutokana na wenzetu.”


“Ili kutoka hapa lazima tufanye juhudi kila linalowezekana kufanya usajili wa wachezaji bora na wenye uwezo wa kuipeleka Simba nusu fainali,”


Wakati huo huo Ahmed Ally amesema kikosi cha Simba SC kinatarajia kuondoka jijini Dar es Salaam leo kuelekea Ruangwa mkoani Lindi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC, utakaopigwa keshokutwa Jumatano (Mei 03( katika Uwanja wa Majaliwa.


Baada ya mchezo huo Simba SC itasafiri kuelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ utakaoikutanisha na Azam FC.


Miamba hiyo itacheza mchezo huo Jumamosi (Mei 06) katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, huku Nusu Fainali nyingine ya Michuano hiyo ikitarajiwa kupigwa Jumapili (Mei 07) kati ya Mabingwa watetezi Young Africans dhidi ya Singida Big Stars katika Uwanja wa CCM Liti mkoani Singida.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post