Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari, Oliveira amesema yeye anapendelea mechi za derby kwa sababu ni mchezo ambao wachezaji, makocha na hata mashabiki wanaupenda
"Tumefanya maandalizi mazuri, wachezaji wako tayari, hii ni mechi kubwa. Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tumejiandaa vyema kusaka ushindi"
"Nawaambia mashabiki wetu waje kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa, uwingi wa mashabiki utatupa nafasi ya kuwa na mchezaji wa 12 uwanjani," alisema Oliveira
Kwa upande wa kikosi, Robertinho amesema wachezaji wake wote wako tayari kwa mchezo huo
Nae nahodha msaidizi wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema mchezo dhidi ya Yanga kesho ni kama fainali kwao kwani wanazihitaji alama zote tatu
Zimbwe Jr amesema wanahitaji ushindi ili kurejesha matumaini katika mbio za ubingwa
"Hii ni mechi kubwa, kwa utamaduni wa Simba na Yanga sio jambo zuri sisi kupoteza mchezo na kuwaruhusu watangaze ubingwa mbele yetu, hivyo hilo linatuhamasisha kuhakikisha tunapambana kwa jasho na damu ili kupata alama tatu"
"Lakini jambo muhimu zaidi kwetu hatutafuti ushindi ili kuizuia Yanga kutwaa ubingwa mbele yetu, bali hata sisi tuko kwenye mbio za ubingwa. Kama hatutapata ushindi tutapunguza nafasi yetu lakini ushindi utatuongezea nafasi kwani tutapunguza gap la pointi"
"Muhimu tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani , tunawaahidi watapata burudani na tumejipanga kushinda," alisema Zimbwe Jr
Post a Comment