Yanga yazindua tawi Mjini Lubumbashi

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Klabu ya Yanga leo imeandika historia kwa kufungua Tawi la kwanza la klabu nje ya Tanzania, katika Mji wa Lubumbashi DR Congo

Uzinduzi wa Tawi hilo la Yanga Wakali Kwanza ulithibitishwa na Rais wa klabu Injinia Hersi Said katika hafla ambayo pia ilihudhuriwa na Makamu wa Rais Arafat Haji, Wajumbe wa Baraza la Wadhamini na uongozi, Mtendaji Mkuu na uongozi wa Yanga Lubumbashi

Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi ambayo Wanachama walikabidhiwa kadi, Hersi alisema Yanga imefungua milango kwa Mashabiki wake wanaoishi nje ya nchi kufungua Matawi 'Virtual Branch' ambayo utaratibu wake wa kufungua umerahisishwa

Yanga iko Libumbashi kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa kesho Jumapili

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post