Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wametangaza viingilio mapema ili kuwapa nafasi mashabiki kuwa na muda wa kutosha kununua tiketi kuepuka changamoto zinazojitokeza siku ya mchezo
Aidha Kamwe amewataka mashabiki kujenga utamaduni wa kununua tiketi zao mapema na sio kusubiri siku ya mchezo na hivyo kukumbana na changamoto zisizotarajiwa
"Tiketi zimeanza kuuzwa mapema ili kuhakikisha mashabiki wananunua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu ambao hujitokeza siku ya mchezo"
"Ni vyema tukaacha mazoea, tujenge utamaduni wa kununua tiketi mapema ili kuondokana na kadhia za dakika za lala salama," alisema Kamwe
Viingilio vya mchezo huo;
VIP A - Tsh 30,000/-
VIP B - Tsh 20,000/-
VIP C - Tsh 15,000/-
Orange - Tsh 10,000/-
Mzunguuko - Tsh 5,000/-
Post a Comment